• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Baraza la chini la bunge la Marekani lapitisha mswada wa ulinzi wa dola za kimarekani bilioni 717

    (GMT+08:00) 2018-05-25 17:50:28

    Baraza la chini la bunge la Marekani jana limepitisha mswada wa ulinzi wa dola za kimarekani bilioni 717, ambazo zitatumika katika kulipa askari, kuongeza meli na ndege za kivita, na kufanya gwaride la kijeshi huko Washington.

    Spika wa baraza hilo Bw. Paul Ryan amesema, mswada huo unasaidia kuimarisha mafunzo ya kijeshi, kuboresha vifaa, kuongeza ukubwa wa jeshi la Marekani, na kuweka kipaumbele kwenye ulinzi wa makombora wakati Marekani inapokabiliwa na tishio la nyuklia.

    Vyombo vya habari vya Marekani vimesema, dola za kimarekani 617 zitatumika kwenye matumizi ya msingi, dola bilioni 69 zitatumika kwenye mfuko wa vita ya dharura katika nchi za nje, na dola bilioni 22 zitatumika kwenye miradi ya silaha za kinyukilia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako