• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • ICPAC yaonya kutokea kimbunga kipya kaskazini mwa Somalia

    (GMT+08:00) 2018-05-25 18:50:44

    Kituo cha Utabiri wa Hali ya Hewa (ICPAC) kilicho chini ya Jumuiya ya maendeleo ya kiserikali ya nchi za Afrika Mashariki IGAD kimeonya kuwa kimbunga kilichopewa jina la Mekuku kinatishia kukumba mkoa unaojiendesha wa Puntland nchini Somalia.

    Kituo hicho kimesema, kinafuatilia kwa karibu kimbunga Mekuku ambacho kinakuja baada ya kimbunga Sagar kilichosababisha mvua na mafuriko mkoani Puntland na watu 25 kufariki katika mkoa wa Somaliland.

    Wakati huohuo, Idara ya Utabiri wa Hali ya Hewa nchini Sudan Kusini imeonya kuwa mikoa kadhaa nchini humo iko hatari kukumbwa na mafuriko kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha. Idara hiyo imesema, mvua kubwa zinatarajiwa kunyesha katika mwezi Juni, Julai na Agosti, na zinaweza kusababisha mafuriko mabaya katika maeneo yanayokumbwa na mafuriko mara kwa mara ya Bahr el Ghazal, Upper Nile na Unity, huku miji ya Bor, Bentou, Aweil na Pibor ikiwa katika hatari kubwa ya kukumbwa na mafuriko hayo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako