• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mkutano wa WHO wafungwa

    (GMT+08:00) 2018-05-27 16:34:32

    Mkutano mkuu wa 71 wa Shirika la Afya Duniani WHO umefungwa jana mjini Geneva, baada ya kupitia mpango wa kimkakati wa miaka mitano ijayo, ambao lengo lake kuu ni "bilioni tatu".

    Katibu mkuu wa WHO Bw. Tedros Adhanom Ghebreyesus amesisitiza umuhimu wa kutimiza lengo la "bilioni tatu", maana yake ni kwamba kuanzia mwaka 2019 hadi 2023, watu wenye bima ya afya duniani wataongezeka kwa bilioni moja, watu wanaoweza kupata huduma bora zaidi wakati wa matukio ya dharura ya afya wataongezeka kwa bilioni moja, na watu wenye afya nzuri zaidi wataongezeka kwa bilioni moja.

    Aidha, mkutano huo pia umepitisha muswada wa mpango wa kampeni ya kuhimiza mazoezi duniani kati ya mwaka 2018 hadi 2030, unaolenga kuhimiza watu wenye umri tofauti kufanya mazoezi, ili kuongeza uwezo wa kujikinga maradhi na kuwa na afya nzuri zaidi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako