• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Maofisa wa Marekani wamewasili Korea Kaskazini kwa ajili ya maandalizi ya mkutano kati ya Rais Trump na Kim

    (GMT+08:00) 2018-05-28 09:51:39

    Rais Donald Trump wa Marekani amethibitisha kuwa kikundi cha maofisa wa Marekani wamewasili nchini Korea Kaskazini kwa ajili ya maandalizi ya mkutano kati yake na kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un.

    Mkutano kati ya viongozi hao wawili ulipangwa kufanyika tarehe 12 Juni nchini Singapore.

    Rais Donald Trump amesema anaamini kuwa Korea Kaskazini ina mustakbali mzuri, na iko siku itakuwa nchi yenye nguvu kiuchumi na kifedha.

    Gazeti la Washington Post limesema balozi wa zamani wa Marekani nchini Korea Kusini Sung Kim amewasili Korea Kaskazini na kukutana na naibu waziri wa mambo ya nje wa Korea Kaskazini Bw. Choe Son Hui.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako