• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • AU wawataka watendaji wa nje kuepuka vitendo vinavyoweza kuharibu maendeleo ya Somalia

  (GMT+08:00) 2018-05-28 10:00:45

  Msemaji wa kamati ya Umoja wa Afrika Bw. Moussa Mahamat ameeleza wasiwasi kuhusu ongezeko la uingiliaji wa nje unaofanywa watendaji wasio wa Afrika katika mambo ya ndani ya Somalia.

  Bw. Faki amesema hayo alipokutana na waziri mkuu wa Somalia Bw. Ali Khaire nchini Ethiopia, na kuongeza kuwa hatua hizo zinatishia kuharibu juhudi za ujenzi wa amani na ujenzi wa taifa zinazoendelea nchini Somalia.

  Amesema uingiliaji huo unahatarisha maendeleo yaliyopatikana kupitia juhudi za pamoja za tume ya AMISOM na jeshi la Somalia. Amezitaka pande za nje kuepuka kuchukua hatua zinazoweza kuharibu mchakato wa maendeleo ya Somalia.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako