• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mashindano ya Magari ya Mwendokasi: Ricciardo wa Australia ashinda mbio za Monaco

    (GMT+08:00) 2018-05-28 10:11:18

    Dereva Dani Ricciardo wa Australia na timu ya Redbull jana ameshinda taji la mbio za Monaco nchini Ufaransa za mashindano ya magari ya mwendokasi baada ya kushika nafasi ya kwanza dhidi ya madereva wenzake.

    Mshindi wa pili kwenye mbio hizo alikuwa mjerumani Sebastian Vettel wa timu ya Ferari na nafasi ya tatu ilikwenda kwa mwingereza Lewis Hamilton wa timu ya Mercedes.

    Ushindi huu kwa Ricciardo unakuwa ni wa pili katika mbio sita zilizokwishafanyika mpaka sasa baada ya kushinda mbio za China mwezi Aprili, hivyo anaingia kwenye kinyanga'anyiro cha ubingwa wa jumla msimu huu kwa kuwa tayari analingana kitakwimu na Lewis Hamilton na Sebastian Vettel ambao pia wameshinda mara mbili kila mmoja.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako