• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mkutano wa nne wa Baraza la Viongozi Vijana wa China na Afrika wafanyika Shenzhen

    (GMT+08:00) 2018-05-28 10:13:13

    Mkutano wa nne wa Baraza la Viongozi Vijana wa China na Afrika ulifanyika Jumamosi na Jumapili mjini Shenzhen, ukiwa na kauli mbiu kuhusu mchango wa vijana katika kutafuta njia ya maendeleo inayolingana na hali ya kitaifa.

    Wanasiasa vijana wapatao 70 kutoka vyama vya siasa 40 katika nchi 40 za Afrika wamehudhuria mkutano huo.

    Waziri wa Mawasiliano ya Nje wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China Bw. Song Tao alihudhuria na kuhutubia ufunguzi wa mkutano huo, akisema Chama cha Kikomunisti cha China na vyama vya kisiasa vya Afrika vyote vinatilia maanani maendeleo ya vijana na kutumai kuwa vijana wa China na Afrika waitikie wito wa zama, kuchangia hekima zao katika kutafuta maendeleo ya nchi, kukuza ushirikiano na urafiki kati ya China na Afrika, na kutoa mchango katika kujenga jumuiya ya binadamu yenye hatma ya pamoja.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako