• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ujumbe wa Marekani wawasili nchini Korea Kaskazini katika hatua mpya ya maandilizi ya mkutano wa viongozi wa nchi hizo

    (GMT+08:00) 2018-05-28 19:02:50

    Rais Donald Trump wa Marekani amesema kuwa ujumbe wa kidiplomasia wa nchi hiyo umewasili nchini Korea Kaskazini ili kuandaa mkutano kati yake na kiongozi wa Korea Kaskazini.

    Katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Twitter, rais Trump amesema anaamini kuwa Korea Kaskazini ina matarajio makubwa na iko siku itakuwa nchi kubwa kiuchumi na kifedha.

    Kuwasili kwa ujumbe wa Marekani kumekuja siku moja baada ya rais wa Korea Kusini Moon Jae-in kufanya mkutano wa ghafla na kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un katika upande wa Korea Kaskazini kwenye kijiji cha Panmunjom.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako