• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Umoja wa Ulaya wasema kulinda makubaliano ya nyuklia ya Iran kunahusiana na usalama wa Ulaya

    (GMT+08:00) 2018-05-29 09:16:28

    Ofisa mwandamizi wa Umoja wa Ulaya anayeshughulikia sera za kidiplomasia na usalama Bibi Federica Mogherini, amesema hatua za umoja wa Ulaya kulinda makubaliano ya nyuklia na Iran, yanatokana na maslahi ya kiusalama na sio ya kiuchumi.

    Bibi Mogherini amesema Umoja wa Ulaya hauoni njia yoyote ya kuwa na usalama kwenye eneo la mashariki ya kati bila kuwepo kwa makubaliano hayo.

    Tangu Rais Donald Trump alipotangaza Marekani kujitoa kwenye makubaliano ya nyuklia ya Iran, Bibi Mogherini amekuwa akisema mara kwa mara kuwa Umoja wa Ulaya utaendelea kuheshimu makubaliano hayo, kama Iran itaendelea kuyaheshimu. Ili kuyalinda makubaliano hayo tarehe 18 Mei, Umoja wa Ulaya ulipendekeza kutumia sheria ya kuyalinda makampuni ya Ulaya yanayofanya biashara nchini Iran baada ya Marekani kutangaza kuiwekea Iran vikwazo tena.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako