• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yakaribisha nchi zote wanachama wa UM kutumia kwa pamoja kituo chake cha anga za juu

    (GMT+08:00) 2018-05-29 09:50:56

    China imetangaza kuwa inakaribisha nchi zote wanachama wa Umoja wa Mataifa kushirikiana na China kutumia kwa pamoja kituo chake cha anga za juu CSS kitakachojengwa katika siku za baadaye.

    Balozi wa China kwenye Umoja wa Mataifa na mashirika mengine ya kimataifa mjini Vienna Bw. Shi Zhongjun, amesema kituo hicho sio kwa ajili ya China tu, bali pia ni kwa ajili ya dunia nzima. Amesema nchi zote bila kujali ukubwa wao na kiwango cha maendeleo, zinaweza kushiriki katika ushirikiano huo kwa usawa.

    Kituo hicho kinachotarajiwa kurushwa kabla ya mwaka 2019, na kukamilisha ujenzi na kuanza kutoa huduma mwaka 2022, kitakuwa ni kituo cha kwanza cha anga za juu kinachojengwa na nchi inayoendelea na kuwa wazi kwa ushirikiano na nchi zote wanachama wa Umoja wa Mataifa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako