• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Soka, Tanzania: Msimu wa Ligi Kuu 2017-2018 wafungwa rasmi jana

  (GMT+08:00) 2018-05-29 10:09:00

  Msimu wa mwaka 2017-2018 wa Ligi kuu ya soka Tanzania Bara umehitimishwa jana kwa mechi nane zilizopigwa kwenye miji tofauti, ambapo vinara wa ligi hiyo Simba ambao ndiyo mabingwa walipata sare ya magoli 1-1 na Majimaji FC, na sasa wamefikisha alama 69.

  Kwa mujibu wa kanuni za ligi hiyo Majimaji na Njombe Mji ndizo timu zilizoshuka daraja kwa ndizo zenye alama chache zaidi kuliko timu zingine katika ligi hiyo.

  Azam FC imefanikiwa kumaliza nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi na jana kwenye mechi yake ya mwisho dhidi ya mabingwa wa mwaka 2016-2017 Yanga walipata ushindi wa magoli 3-1.

  Katika matokeo mengine ya jana, Kagera Sugar ilipata ushindi wa 2-1 mbele ya wenyeji, Lipuli FC mjini Iringa, na Tanzania Prisons ikiwa nyumbani mjini Mbeya iliilaza Singida United kwa goli 1-0. Mtibwa Sugar ilitoka sare ya 0-0 na Mbeya City mjini Morogoro, Mwadui FC iliwashinda wenyeji wake Njombe Mji FC 2-0 na Mbao FC ikatoka sare ya 1-1 na Ruvu Shooting Uwanja wa CCM Kirumba mjini Mwanza.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako