• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Biashara kupitia mtandao wa internet nchini China wafikia dola za kimarekani trilioni 4.5 mwaka jana

    (GMT+08:00) 2018-05-29 19:38:35

    Thamani ya biashara kupitia mtandao wa internet nchini China kwa mwaka jana ilifikia dola za kimarekani trilioni 4.5, ikiwa ni ongezeko la asilimia 11.7 ikilinganishwa na mwaka 2016.

    Hayo yamo kwenye ripoti iliyotolewa leo na Wizara ya Biashara ya China katika mkutano wa mwaka 2018 wa biashara kupitia mtandao uliofanyika hapa Beijing. Ripoti hiyo pia imesema, thamani ya bidhaa zilizouzwa kupitia mtandao wa internet ilifikia dola za kimarekani trilioni 2.6 mwaka jana, ikiwa ni onngezeko la asilimia 21 ikilinganishwa na mwaka 2016.

    Ofisa wa idara ya biashara kupitia mtandao na mawasiliano iliyo chini ya Wizara ya Biashara ya China Qian Fangli amesema, biashara hiyo imeongoza uchumi wa kidijitali wa China na kusaidia kuondokana na umasikini kwenye maeneo ya vijijini mwaka jana.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako