• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rwanda yahimiza kampeni ya kutoa elimu kuhusu madhara ya taka za plastiki

    (GMT+08:00) 2018-05-30 09:13:21

    Rwanda imezindua kampeni ya kitaifa ya kueneza ufahamu kuhusu madhara ya taka za plastiki kwa binadamu, wanyama, samaki na mazingira.

    Kampeni hiyo inayoitwa "pambana na uchafuzi wa plastiki" imeanza jana na itaendelea hadi jumamosi. Mbali na kutoa ufahamu kuhusu hatari za takataka za plastiki, kampeni hiyo pia itahusu kuihamasisha sekta binafsi kuwekeza kwenye mifuko mbadala iliyo rafiki kwa mazingira.

    Waziri wa Mazingira wa Rwanda Bw. Vincent Biruta amesema nchi zote duniani zinachukua hatua kupambana na uchafuzi wa plastiki, Rwanda ni mtangulizi wa juhudi hizi na itaendelea kushirikiana na wadau wengine wa maendeleo na biashara, ili kupata suluhisho endelevu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako