• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • WHO ina matumaini mazuri kuhusu mwitikio wa chanjo ya Ebola nchini DRC

    (GMT+08:00) 2018-05-30 17:51:34

    Shirika la Afya Duniani (WHO) limesema kuwa ingawa watu walioko hatarini zaidi wamepata chanjo nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), bado linatoa hadhari kuhusu maendeleo ya Ebola nchini humo.

    Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Dharura ya Shirika hilo Peter Salam amesema, zaidi ya watu 400 nchini DRC ambao wako hatarini kuambukizwa Ebola wamepewa chanjo, na kwamba zoezi la kutoa chanjo hiyo kwenye mji wa kaskazini magharibi wa Mbandaka nchini humo lilienda vizuri.

    Amesema mpaka sasa hakuna kesi zilizoongezeka za maambukizi ya ugonjwa huo, ambayo ni hatua nzuri, na kwamba mikoa ya ndani zaidi ya Iboko na Bikoro inafuata kwenye mkakati wa kutoa chanjo.

    Takwimu za hivi karibuni zilizotolewa na WHO zinaonyesha kuwa, mpaka kufikia May 21, jumla ya kesi 58 za Ebola, ikiwemo vifo 27, viliripotiwa nchini humo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako