• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Serikali ya Tanzania yatoa wito kwa Benki kutoa mikopo itkayowezesha ukuaji wa sekta za viwanda na Kilimo

    (GMT+08:00) 2018-05-30 19:41:18

    Serikali ya Tanzania imeitaka sekta ndogo ya benki kuongeza ubunifu kwa kutoa mikopo ya muda mfupi na mirefu ambayo itawezesha ukuaji wa sekta za viwanda na kilimo pamoja na wajasiriamali wadogo.

    Hayo yalisemwa jana jijini Dodoma na Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT),Prof Florens Luoga,kwa niaba ya Waziri wa Fedha na Mipango,Dk Philip Mpango,katika mkutano wa wadau wa sekta ya fedha uliowashirikisha wabunge,washirika wa maendeleo,wakuu wa taasisi za fedha,na Wizara ya Fedha na Mipango.

    Prof Luoga alitoa wito huo kufuatia kuwapo kwa changamoto katika sekta hiyo ikiwamo ukosefu wa uwekezaji wa miradi mikubwa ya maendeleo katika viwanda,kilimo,miundombinu,na ukosefu wa mikopo kwa wajasiriamali wadogo na wa kati.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako