• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania-Wadudu waharibu mazao

    (GMT+08:00) 2018-05-30 19:48:42

    Zaidi ya hekta 17,339 za mazao ya chakula na biashara katika wilaya ya Kilosa,mkoani Morogoro yameshambuliwa na wadudu waharibifu,hali inayoleta hofu kubwa kwa wakulima wa maeneo hayo.

    Wadudu hao waharibifu ni viwavi jeshi vamizi,,kangambili,vidukari,panya,na ndege aina ya kweleakwelea.

    Ofisa Kilimo Umwagiliaji na Ushirika wa wilaya ya Kilosa,Tatu Kachenje,alisema mazao yaliyoathiriwa zaidi ni mpunga,mahindi,na pamba,ambapo licha ya kunyunyizia dawa mbalimbali,wadudu hao wameendelea kufanya uharibifu mkubwa.

    Aidha Tatu alieleza kuwa kata 29 zinazolimwa mahindi,mpunga na pamba zimevamiwa na viwavijeshi vamizi na kusababisha hasara kubwa kwa wakulima na kuleta hofu ya kuwapo upungufu wa chakula katika maeneo hayo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako