• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Zimbabwe yatangaza wananchi wanaoishi nje ya nchi hawataweza kupigia kura uchaguzi

    (GMT+08:00) 2018-05-31 09:51:46

    Mahakama ya katiba Zimbabwe imetangaza kuwa wazimbabwe wanaoishi nje ya nchi hawawezi kupigia kura uchaguzi uliopangwa kufanyika Julai 30 mwaka huu.

    Uamuzi huo umekuja baada ya baadhi ya wazimbabwe wanaoishi ng'ambo wanaowakilishwa na Shirika la wanasheria wa Zimbabwe kuhusu haki za kibinadamu ZLHR, kutoa ombi kwa mahakama, wakidai kuwa katiba mpya iliyopitishwa mwaka 2013 inawaruhusu wapige kura kutoka nje ya nchi.

    Lakini naibu jaji mkuu wa nchi hiyo Bibi Elizabeth Gwaunza amesema ombi hilo halina msingi wowote na hivyo limefutwa.

    Mfumo wa sasa wa kupigia kura nchini Zimbabwe unataka wapiga kura wapige kura ndani ya nchi katika kituo kilichowekwa katika eneo wanakoishi. Lakini pia unawaruhusu wanaotoa huduma kwa serikali nje ya nchi kupiga kura.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako