• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Zaidi ya nusu ya watoto duniani wanakabiliwa na tishio la vita, umasikini na kutengwa kijinsia

  (GMT+08:00) 2018-05-31 18:09:03

  Ripoti iliyotolewa na shirika la hisani la Save the Children imesema, zaidi ya nusu ya watoto duniani wanakabiliwa na tishio la umasikini, mapigano, au kutengwa kwa watoto wa kike.

  Ripoti hiyo iliyotolewa siku moja kabla ya Siku ya Kimataifa ya Watoto inayoadhimishwa Juni Mosi, imeeleza jinsi mambo hayo matatu makubwa yanavyowakosesha watoto utoto wao duniani. Ripoti hiyo imegundua kuwa zaidi ya watoto bilioni moja wanaishi kwenye nchi zinazokumbwa na umasikini, watoto 240 milioni wanaishi kwenye nchi zinazoathiriwa na vita na ukosefu wa amani, na zaidi ya watoto wa kike milioni 575 wanaishi kwenye nchi ambazo upendeleo wa kijinsia ni suala kubwa.

  Shirika hilo limetoa wito kwa serikali za nchi mbalimbali duniani kutimiza ahadi zilizotoa kwenye Umoja wa Mataifa ili kuhakikisha kila mtoto anakwenda shule, analindwa, na ana afya nzuri itakapofika mwaka 2030.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako