• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa China ajibu barua ya wanafunzi wa shule ya msingi ya kijiji cha Zhaojin

    (GMT+08:00) 2018-05-31 18:25:06

    Rais Xi Jinping wa China amejibu barua kutoka kwa wanafunzi wa shule ya msingi ya Beiliang iliyoko katika kijiji cha Zhaojin, mkoani Shaanxi na kuwatakia watoto wote heri ya Siku ya Kimataifa ya Watoto.

    Kwenye barua yake, rais Xi amesema, alifurahi kupata barua kutoka kwa wanafunzi hao ambayo imesema, wazee wa kijiji hicho huwajulisha historia ya mapinduzi ya kijiji hicho. Anatarajia watoto hao kujifunza zaidi historia ya mapinduzi, mageuzi na ujenzi wa China, kuiga mambo mazuri, kupenda chama, taifa na watu wengine, na kuchukua hatua halisi kurithisha tabia nzuri ya kimapinduzi.

    Rais Xi pia amesema, chini ya msaada wa chama na serikali ya mkoa, shule hiyo imekuwa ya kisasa. Anatarajia wanafunzi hao kuthamini mazingira mazuri ya kujifunza na kujitahidi zaidi katika masomo ili kutoa mchango katika kujenga taifa, jamii na kusaidia watu katika siku za baadaye.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako