Mjumbe maalumu wa China anayeshughulikia suala la Mashariki ya Kati Bw. Gong Xiaosheng amesisitiza kuwa Palestina na Israel zinapaswa kusitisha mara moja mapambano, na kurejea mapema kwenye meza ya mazungumzo, ambayo ni njia pekee ya kutatua mgogoro kati ya nchi hizo mbili kwa njia ya kisiasa. Bw. Gong ambaye yuko ziarani nchini Misri amesema China inaona jumuiya ya kimataifa inapaswa kuendelea kusukuma mbele Mpango wa Nchi Mbili, na kuendelea na juhudi za kiujenzi za kuhimiza utatuzi wa kisiasa wa suala la Palestina, kwa mujibu wa maazimio ya Umoja wa Mataifa na makubaliano husika ya kimataifa.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |