• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wang Yi asema China na Ujerumani zapaswa kushirikiana katika kulinda utulivu wa dunia dhidi ya hatua za upande mmoja na za kujilinda kibiashara

    (GMT+08:00) 2018-06-01 10:18:56

    Waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Wang Yi amesema China na Ujerumani zinapaswa kushirikiana katika kulinda utulivu wa dunia wakati hatua za upande mmoja na za kujilinda kibiashara zikiongezeka siku hadi siku.

    Bw. Wang Yi amesema hayo katika mkutano wa pamoja na waandishi wa habari akiwa na mwenzake wa Ujerumani Bw. Heiko Maas mjini Berlin. Amesema China na Ujerumani zikiwa ni nchi za kuwajibika na wenzi wa kimkakati, zinapaswa kushirikiana katika kuleta ushawishi chanya na kusaidia kulinda utulivu wa dunia.

    Siku hiyo akikutana na Bw. Wang Yi, rais Steinmeir wa Ujerumani amesema pande hizo mbili zinapaswa kuimarisha ushirikiano, kufanya juhudi katika kulinda amani na utulivu duniani, na kukuza maendeleo ya uchumi wa dunia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako