• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mahakama ya Katiba Burundi yakubali matokeo ya kura za maoni kuhusu katiba

    (GMT+08:00) 2018-06-01 10:34:14

    Mahakama ya Katiba ya Burundi imeidhinisha matokeo ya kura za maoni kuhusu marekebisho ya katiba, yatakayorefusha muda wa rais kuwa madarakani kutoka miaka mitano hadi miaka saba na kumruhusu rais kuhudumu kwa mihula miwili mfululizo.

    Tume Huru ya Uchaguzi ya Burundi ilitangaza ijumaa iliyopita kuwa asilimia 73.26 ya wapiga kura wanakubali marekebisho mapya katika upigaji kura za maoni uliofanyika Mei 17. Matokeo hayo yaliwasilishwa kwa Mahakama ya Kati kwa ajili ya kupitishwa na kutangazwa rasmi.

    Mkuu wa Mahakama ya Katiba Bw. Charles Ndagijimana amesema hakuna dosari kubwa zinazoweza kuathiri matokeo hayo. Pia amesema mahakama hiyo inaona zoezi hilo la kura za maoni linaendana na sheria ya Burundi, na malalamiko yaliyotolewa na muungano wa vyama vya upinzani Burundians' Hope, kuhusiana na kanuni na matokeo ya upigaji kura, hayana msingi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako