• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania kutoa fidia kwa watu ambao ardhi zao zimetumiwa na jeshi

    (GMT+08:00) 2018-06-01 10:35:53

    Serikali ya Tanzania imetenga dola za kimarekani milioni 10 kwa ajili ya kutoa fidia kwa watu ambao ardhi zao zimetumiwa na Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).

    Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dk. Hussein Mwinyi ameliambia bunge kuwa watu hao watapewa fidia mara baada ya pesa kutolewa na Wizara ya Fedha. Amekiri kuwa serikali ilifahamu matumizi ya ardhi katika vijiji vilivyotajwa na kwamba tathmini kwa fidia ilifanywa mwaka 2013.

    Dk. Mwinyi aliliambia bunge kuwa serikali ilichukua hatua kutatua migogoro ya ardhi kati ya vijiji na kambi za jeshi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako