• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Baraza la Usalama la UM larefusha muda wa vikwazo dhidi ya Sudan Kusini

    (GMT+08:00) 2018-06-01 10:36:17

    Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limepitisha azimio lililotolewa na Marekani la kurefusha muda wa vikwazo dhidi ya Sudan Kusini, baada ya nchi tisa wajumbe kupiga kura za ndio na wengine sita kutopiga kura.

    Azimio hilo nambari 2418 limeamua kuendelea kupiga marufuku ya usafiri na kuzuia mali dhidi ya watu binafsi na mashirika yaliyoamuliwa mpaka tarehe 14, Agosti mwaka 2018.

    Wakati huohuo, Jumuiya ya Maendeleo ya Kiserikali ya Afrika Mashariki IGAD imetaka pande hasimu nchini Sudan Kusini kutekeleza makubaliano ya kusimamisha vita na kuacha kutumia silaha. Pia imesema IGAD itawachukulia hatua wale watakaokiuka makubaliano ya kusitisha uhasama yaliyosainiwa upya mwezi Disemba mwaka 2017.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako