• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Marekani kupiga kura ya veto muswada wa Kuwait kuhusu ulinzi wa Palestina

  (GMT+08:00) 2018-06-01 18:35:30

  Balozi wa Marekani kwenye Umoja wa Mataifa Nikki Haley, amesema Marekani itapiga kura ya veto muswada wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa ulioandaliwa na Kuwait kuhusu ulinzi wa raia wa Palestina.

  Bi. Haley amesema muswada huo una mtazamo wa upande mmoja ambao utasaidia kupunguza juhudi zinazoendelea za kuleta amani kati ya Israel na Palestina.

  Kuwait, ambayo sio mjumbe wa kudumu wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, imesambaza muswada huo kwa nchi wajumbe wiki mbili zilizopita.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako