• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wilaya zatakiwa kutekeleza agizo la viwanda 100

    (GMT+08:00) 2018-06-01 19:15:31

    Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Alexander Mnyeti ameziagiza Halmashauri za Wilaya za Mkoa huo kuhakikisha zinatekeleza agizo la uanzishwaji wa viwanda 100 litekelezwa hadi mwezi Septemba, mwaka huu.

    Mnyeti ametoa agizo hilo wakati akizungumza na watumishi na viongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Babati, wiki hii huku akiziwekea halmashauri zote za wilaya malengo ya kuwa na viwanda 15.

    Mnyeti alisema serikali ilitoa agizo la kila mkoa uanzishe viwanda 100 hivyo na mkoa wa Manyara nao unapaswa kuhakikisha unatekeleza agizo hilo kwa kila halmashauri kuwa na viwanda 15.

    Alisema agizo hilo linatakiwa kutekelezwa kwa kila sekta ikiwemo kilimo na mifugo ambazo ndizo shughuli kuu za kiuchumi kwa wananchi wengi wa mkoa huo. Aliwapongeza mkuu wa wilaya hiyo Mhandisi Raymond Mushi na mkurugenzi mtendaji wa halmashauri hiyo Hamis Malinga kwa kuanza kutekeleza agizo hilo la uanzishwaji wa viwanda vipya.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako