• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • China yapongeza taarifa ya pamoja ya Russia na Korea Kaskazini kuhusu kutokuwepo kwa silaha za nyuklia kwenye peninsula ya Korea

  (GMT+08:00) 2018-06-01 19:20:45

  Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bibi Hua Chunying amesema China inapongeza taarifa iliyotolewa na Russia na Korea Kaskazini kuhusu kutokuwepo kwa silaha za nyuklia kwenye peninsula ya Korea, na kuitaka Russia kuendelea na mchakato mzuri wa kutatua suala la nyuklia la peninsula ya Korea kwa njia ya kisiasa.

  Bibi Hua Chunying amesisitiza kuwa China inafurahi kuona uhusiano wa pande mbili unaendelezwa na kuimarisha mawasiliano kati ya viongozi wa Korea kaskazini na Russia, ikiamini kuwa kufanya hivyo kutasaidia kuhimiza mchakato wa utatuzi wa suala la peninsula ya Korea kwa njia ya kisiasa na kulinda amani na utulivu wa peninsula ya Korea na eneo la Asia ya Kaskazini na Mashariki.

  Habari zinasema, Waziri wa mambo ya nje wa Russia Bw. Sergey Lavrov alifanya ziara nchini Korea Kaskazini na kukutana na kufanya mazungumzo na kiongozi wa nchi hiyo Kim Jong-un.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako