• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais Trump asema atakutana na kiongozi wa Korea Kaskazini kama ilivyopangwa

    (GMT+08:00) 2018-06-02 18:08:16

    Rais Donald Trump wa Marekani amesema kwamba atakutana na kiongozi wa Korea Kaskazini Bw. Kim Jong-un huko nchini Singapore mnamo tarehe 12 mwezi Juni kama ilivyopangwa.

    Wakati Rais Trump alipokutana na Makamu wa Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Chama cha Wafanyakazi wa Korea Kaskazini Bw. Kim Yong Chol katika ikulu ya Marekani, pande hizo mbili zimejadili karibu matatizo yote ikiwa ni pamoja na mkutano wa viongozi wa Marekani na Korea Kaskazini, vikwazo vya Marekani dhidi ya Korea Kaskazini na masuala mengine. Rais Trump amesifu jukumu la China katika kukuza mazungumzo ya Marekani na Korea Kaskazini na kuamini kwamba Korea Kaskazini ina nia dhati ya ya kuondoa silaha za nyuklia katika peninsula ya Korea, na Marekani na Korea Kaskazini hatimaye zinaweza kufikia matokeo mazuri kwa kupitia jitihada.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako