• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Waziri Mkuu wa Sudan aeleza mchango wa nchi yake kwa IGAD katika mchakato wa amani ya Sudan Kusini

    (GMT+08:00) 2018-06-02 18:11:42

    Waziri mkuu wa Sudan, El-Dardiri Mohamed Ahmed, amerudia kuzungumzia mchango mkubwa wa nchi yake kwa IGAD katika maendeleo ya mchakato wa amani ya Sudan Kusini.

    El-Dardiri aliyasema hayo jana mjini Addis Ababa wakati wa mkutano wake na mwenyekiti wa baraza la mawaziri wa nchi za pembe ya Afrika ambaye pia ni waziri wa mambo ya nje wa Ethiopia Workneh Gebeyehu.

    Siku ya alhamis, El-Dardiri alihudhuria mkutano mkuu wa 62 wa baraza la mawaziri wa IGAD, uliofanyika mjini Addis Ababa, ambapo washiriki walitoa wito kwa pande za kisiasa za Sudan Kusini kusitisha vurugu na ukatili na kudumisha amani.

    Katika hatua nyingine, El-Dardiri na Gebeyehu walizungumza kuhusu kuimarisha uhusiano kati ya Ethiopia na Sudan.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako