• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Jambo muhimu la utekelezaji wa makubaliano yaliyofikiwa Washington ni kuendana na mwelekeo wa pamoja

    (GMT+08:00) 2018-06-03 16:54:11

    Ujumbe wa China unaoongozwa na mjumbe wa ofisi ya siasa ya kamati kuu ya chama cha kikomunisti cha China, naibu waziri mkuu wa China Bw. Liu He pamoja na ujumbe wa Marekani unaoongozwa na waziri wa biashara wa Marekani Wilbur L. Ross tarehe 2 hadi tarehe 3 Juni wamefanya mazungumzo mjini Beijing kuhusu suala la uchumi na biashara kati ya nchi hizo mbili.

    Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na China, pande mbili zimejadili kuhusu utekelezaji wa makubaliano yaliyofikiwa kati ya pande mbili hizo mjini Washington, katika kilimo, nishati na sekta nyingine, na kupata maendeleo, mambo halisi yanatarajiwa kuthibitishwa na pande mbili.

    Kama ilivyoandika kwenye taarifa ya China, matokeo yaliyofikiwa kati ya China na Marekani, yanapaswa kuwa na msingi wa pande mbili kuendana na mwelekeo wa pamoja na kutoanzisha vita vya biashara, kama vile Marekani kuweka vikwazo vya kibiashara kama kutoza ushuru, matokeo yote yanayofikiwa kati ya pande hizo mbili hayatatekelezwa. Huu ndio msimamo wa China, pia ni jambo muhimu la kuhakikisha utekelezaji wa makubaliano yaliyofikiwa mjini Washington.

    Kauli hiyo ya China inatokana na sababu yake. Kwani Siku kadhaa kabla ya Bw. Ross kuja China, Marekani ilibadili msimamo wake na kutangaza kutoza ushuru wa asilimia 25 kwa bidhaa muhimu za teknolojia ya viwanda za China zenye thamani ya dola za kimarekani bilioni 50. Vilevile habari kutoka kwenye baadhi ya vyombo vya habari zinasema kuwa, kama ujumbe wa Marekani uliofika Beijing awali hautafikiwa na China, Bw. Ross hatakuja China. Lakini ukweli ni kwamba, Bw. Ross anakuja Beijing kabla ya muda uliopangwa, pia ana hamu kubwa ya kufanya mazungumzo na China. Hii inaonyesha kwamba, kufanya mazungumzo huku tofauti za kibiashara ni hali ya kawaida ya mazungumzo ya uchumi na biashara kati ya China na Marekani.

    Bw. Ross amesema mazungumzo hayo ni ya kirafiki na wazi. Lakini mambo halisi hayajathibitishwa, haijulikani kutatokea nini. Kwa hivyo China iko tayari kukabiliana na hali yoyote.

    Lengo la mageuzi na kufungua mlango ya China ni dhahiri, hatua yake ni ya umadhubuti. Kuongeza uagizaji bidhaa kutoka nje, na kupanua kigezo cha kuruhusu kuingia soko la China, zote zinatokana na kuridhisha mahitaji ya maisha mazuri ya watu wa China na kutimiza maendeleo ya uchumi yenye sifa bora. Huu ni uamuzi wa kimkakati, hautabadilika kutokana na shikinizo la nje.

    Kwa umuhimu wa makubaliano yaliyofikiwa mjini Washington, China na Marekani zitafanya majadiliano kuhusu namna ya kufanya ushirikiano katika sekta ya uzalishaji, viwanda vya tenkolojia ya juu na bidhaa za huduma. Juhudi za China ni kwa ajili ya kulinda maslahi ya wananchi wa nchi hizo mbli, Marekani itafikiria kuhusu watu wake au la, itaonyeshwa kama inavyoendana na China kwa mwelekeo wa pamoja.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako