• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Algeria yamwita balozi wa Umoja wa Ulaya kutoa malalamiko kuhusu kauli dhidi ya rais wake

    (GMT+08:00) 2018-06-04 09:08:36

    Balozi wa Umoja wa Ulaya nchini Algeria Bw. John O'Rouk ameitwa na wizara ya mambo ya nje ya Algeria, kufuatilia video moja iliyotolewa nchini Ubelgiji na aliyekuwa mtangazaji wa televisheni ya taifa ya Algeria, yenye lugha ya kumkosoa Rais Abdelaziz Bouterflika.

    Katibu mkuu wa wizara ya mambo ya nje wa Algeria Bw. Nourdine Ayadi amesema Algeria inatumai kuwa Umoja wa Ulaya utapinga wazi vitendo kama hivyo na kutaka umoja huo uchukue hatua dhidi ya vitendo visivyo vya uwajibikaji vya mtangazaji huyo.

    Taarifa iliyotolewa na wizara ya mambo ya nje ya Algeria inasema, balozi wa Algeria kwenye Umoja wa Ulaya pia amepewa maelekezo na wizara ya mambo ya nje ya Algeria kuchukua hatua zinazostahili kwa vyombo vinavyohusika vya Umoja wa Ulaya.

    Kumekuwa na maoni tofauti kuhusu hatma ya kisiasa ya rais Abdelaziz Bouterflika, muungano tawala wa vyama vya FLN na RND umemtaka Rais huyo agombee urais kwa awamu ya tano, na upinzani unataka ajiuzulu. Rais Bouterflika amekuwa mgonjwa tangu mwaka 2013 alipokumbwa na kiarusi, na sasa hawezi kutembea wala kuongea kwa sauti.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako