• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Soka, Michuano ya SportPesa: Yanga na JKU zashindwa kufuzu raundi ya pili

    (GMT+08:00) 2018-06-04 09:48:24

    Timu mbili za Tanzania, Yanga na JKU zimeondolewa kwenye mashindano ya SportPesa Super Cup baada ya kushindwa kwenye mechi zao za kwanza kwenye michuano hiyo inayoendelea nchini Kenya.

    YANGA ya Dar es Salaam imeondolewa kunako hatua ya kwanza tu ya michuano hiyo kufuatia kichapo cha mabao 3-1 kutoka kwa Kakamega Homeboyz ya Kenya kwenye Uwanja wa Afraha mjini Nakuru.

    Kwa upande wao JKU kutoka Zanzibar imefungwa kwa magoli 3-0 na mabingwa watetezi, Gor Mahia ya Kenya.

    Michuano hiyo inaendelea leo ambapo Simba ya Tanzania watatupa mguu wao wa kwanza kwa kucheza na Kariobangi Sharks ya Kenya mchana, na baadaye Singida United ya Tanzania itamenyana na AFC Leopards ya Kenya jioni.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako