• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Raga, Kimataifa: Kenya yashinda Ubingwa wa London

    (GMT+08:00) 2018-06-04 09:48:41

    Timu ya taifa ya Kenya ya mchezo wa Raga kwa wachezaji 7, imefanikiwa kushinda Ubingwa wa kimataifa wa London baada kuifunga Wales kwenye mchezo wa fainali kwa alama 33-19 kwenye uwanja wa Twickenham.

    Ushindi mnono wa Kenya ulichagizwa na wachezaji Jeffrey Oluoch na Collins Injera waliotengeneza alama mbili za mkupuo kila mmoja, huku William Ambaka na Eden Agero wakiondoka na alama moja kila mmoja.

    Kwa ushindi huo, Kenya sasa imejongezea alama za jumla kwenye msimamo wa dunia ambapo sasa inafikisha 103, ambazo hata hivyo zimebaki kuwa pungufu ili kupanda kwa nafasi ya ubora wa viwango, hasa baada ya Uingereza nayo kushinda nafasi ya tatu kwenye mashindano hayo kwa kuifunga Ireland.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako