• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Moshi mchafu unaotolewa na magari ni chanzo kikubwa cha uchafuzi wa hewa

    (GMT+08:00) 2018-06-04 18:30:37

    Ripoti iliyotolewa hivi karibuni na Wizara ya Ikolojia na Mazingira ya China imesema, moshi mchafu unaotolewa na magari umekuwa chanzo kikubwa cha uchafuzi wa hewa nchini China, na hatua za haraka zinatakiwa kuchukuliwa kudhibiti hali hiyo.

    Ripoti hiyo imesema, China imeendelea kuwa nchi yenye magari mengi zaidi duniani, ikiwa na karibu magari milioni 310, ambayo ni ongezeko la asilimia 5.1 ikilinganishwa na mwaka 2016. Baadhi ya miji imeshuhudia kuongezeka kwa uchafuzi wa hewa kutokana na mchanganyiko wa uchomaji wa makaa ya mawe na moshi mchafu unaotolewa na magari.

    Uchunguzi uliofanywa kwenye miji ya Beijing, Tianjin, Shanghai na miji mingine 12 nchini China umegundua kuwa, moshi unaotolewa na magari umechangia kuanzia asilimia 13.5 hadi 52.1 ya vyanzo vya uchafuzi.

    Wizara hiyo inaandaa muswada wa mpango wa kazi wa kukabiliana na magari yanayotumia dizeli, ambayo yanashukiwa kuwa na kiwango kikubwa cha uchafuzi wa hewa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako