• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Magufuli: Siridhishwi na utendaji wa Benki ya Kilimo

    (GMT+08:00) 2018-06-04 20:31:52

    Rais Magufuli amesema kuwa hajaridhishwa na utendaji wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo (TADB) kwani pamoja na serikali kutoa Sh bilioni 60 kwa ajili ya kukopesha wakulima, taasisi hiyo haijafanya hivyo.

    Badala yake, kwa mujibu wa Rais, TADB imeingia kwenye biashara ya kukopesha benki nyingine na kununua dhamana za serikali huku takribani Sh bilioni 5 iliyotengwa kwa ajili ya kukopeshwa wakulima, haijatolewa hadi sasa.

    Hata hivyo, Rais Magufuli amesema kuwa anatambua lengo la TADB kukopesha fedha hizo ni kuongeza mtaji lakini ameikumbusha taasisi hiyo iliyoundwa kwa lengo la kuinua sekta ya kilimo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako