• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kombe la Dunia, Bado siku 9: Kocha wa Ujerumani aishtua dunia kwa kumwacha Leroy Sane, atoa sababu

    (GMT+08:00) 2018-06-05 09:54:29

    Timu zote 32 zinazoshiriki michuano ya kombe la dunia mwaka huu zimekamilisha zoezi la kuwasilisha majina 23 ya wachezaji kulingana na kanuni ya FIFA, ambayo ilipanga Juni 4 kuwa siku ya mwisho.

    Mataifa yaliyowasilisha majina kamili katika siku ya mwisho inaaminika kuwa makocha walipata changamoto kwenye kuchagua wachezaji, yaani aachwe nani au achukuliwe nani, kwa kuwa tayari kulikuwa na mataifa mengine yaliyokwisha kuwasilisha vikosi vyake hata kabla ya Juni 4.

    Miongoni mwa mataifa yaliyochelewa ni Ujerumani ambapo kocha Joachim Low alipeleka kikosi cha wachezaji 23, kikiwa na nyota wengi wanaocheza soka safi, lakini pia akiiachia dunia mshangao baada ya kuwaacha baadhi.

    Mjadala kwenye majukwa mbalimbali tangu kocha atangaze kikosi chake ilikuwa ni kuhusu kuachwa kwa mchezaji chipukizi machachari Leroy Sane anayecheza kwenye klabu ya Manchester City ya Uingereza.

    Wengi wakidai hakuwa na sababu, lakini yeye akisema kuwa angependa kwenda naye sana, lakini kutokana na nafasi anayocheza mchezaji huyo, kutokana na hazina ya wachezaji waliopo katika Ujerumani na kwa kuwa yeye bado ni kinda, na kwa sababu nafasi za FIFA ni finyu.

    Sane ambaye anacheza nafasi ya kiungo mshambuliaji na nafasi ya winga wa kushoto, nafasi yake sasa itazibwa na wachezaji wa wafuatao: Sami Khedira (Juventus/ITA), Julian Draxler (Paris Saint-Germain/FRA), Toni Kroos (Real Madrid/ESP), Mesut Ozil (Arsenal/ENG), Thomas Mueller (Bayern Munich), Sebastian Rudy (Bayern Munich), Julian Brandt (Bayer Leverkusen), Ilkay Gundogan (Manchester City/ENG), Leon Goretzka (Schalke 04), Marco Reus (Borussia Dortmund).

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako