• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Katibu mkuu wa UM alaani mauaji ya mlinzi wa amani nchini CAR

    (GMT+08:00) 2018-06-05 10:06:25

    Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Antonio Guterres amelaani mauaji ya mlinzi wa amani wa Umoja wa Mataifa kutoka Tanzania, aliyeuawa kwenye shambulizi lililofanywa Juni 3 dhidi ya walinzi amani wa Tume ya Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati MINUSCA, walinzi wengine saba walijeruhiwa.

    Taarifa hiyo imesema Bw. Guterres ametoa heshima kwa walinzi wote waliojitolea mhanga kwa ajili ya amani nchini CAR. Pia ametoa salamu za rambirambi kwa familia ya mfiwa, pamoja na serikali ya Tanzania, na kuwatakia majeruhi wapone haraka.

    Amesema mashambulizi dhidi ya walinzi amani wa Umoja wa Mataifa yanaweza kuchukuliwa kuwa ni uhalifu wa kivita, na vikwazo vitaweza kuwekwa dhidi ya washambuliaji. Ametaka mamlaka za CAR kufanya juhudi zote kufanya uchunguzi ili kuwafikisha wahusika mbele ya sheria.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako