• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kiongozi mkuu wa Iran aamuru maandalizi ya kurutubisha madini ya Uranium

    (GMT+08:00) 2018-06-05 10:06:56

    Kiongozi mkuu wa Iran Ayatollah Ali Khamenei ametaka Shirika la Nishati ya Atomiki la Iran AEOI kujiandaa kurutubisha madini ya Uranium.

    Ayatollah Khamenei ametoa agizo hilo kwenye hotuba yake aliyoitoa kwenye televisheni jana ili kuadhimisha miaka 29 tangu kufariki mwasisi wa Iran Imam Khomeini. Amesema inaonekana kuwa baadhi ya serikali za Ulaya zinatarajia kuwa Iran itakubali vikwazo na kuacha shughuli za nyuklia.

    Iran inafanya majadiliano na nchi za Ulaya kuhusu kuokoa makubaliano ya nyuklia ya Iran baada ya Marekani kujitoa. Kwa mujibu wa makubaliano hayo, Iran inaweza kurutubisha uranium katika ngazi ya asilimia 3.5.

    Wakati huohuo, waziri mkuu wa Israel Bw. Netanyahu anaendelea na ziara yake barani Ulaya kuwashawishi washirika wake kuitikia mwito wake wa kubadilisha makubaliano ya nyuklia ya Iran. Chansela wa Ujerumani Bibi Angela Merkel na Bw. Netanyahu wamekubaliana kuhusu kuizuia Iran kutengeneza silaha za nyuklia, lakini wana maoni tofauti katika jinsi ya kutimiza lengo hilo. Bibi Merkel ameahidi kudumisha makubaliano hayo licha ya Marekani kujitoa, ili kuizuia Iran kumiliki silaha za nyuklia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako