• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Watafiti wa China watengeneza rasilimali ya kuondoa uchafuzi wa metali kwa takataka za kadibodi

    (GMT+08:00) 2018-06-05 16:25:56

    Habari kutoka idara ya biolojia ya kiteknolojia na uhandisi wa kilimo ya taasisi ya sayansi ya China zinasema kikundi kinachoongozwa na mtafiti Wu Zhengyan wa idara hiyo kimevumbua rasilimali ya mseto inayoweza kuondoa uchafuzi wa metali nzito majini kwa ufanisi mkubwa kwa kutumia takataka za kadibodi, na kutoa taswira mpya kwa kushughulikia uchafuzi wa metali na mzunguko wa takataka za kadibodi. Uvumbuzi huo umetolewa kwenye jarida la Langmuir la Marekani.

    Hivi sasa uchafuzi wa metali nzito majini unatokea mara kwa mara, miongoni mwa metali hizi, Hexavalent chromium ni metali ya kawaida inayodhuru vibaya afya ya watu, na teknolojia ya kuondoa uchafuzi wa metali hiyo kwa ufanisi mkubwa na bei nafuu inahitajika sana.

    Hivi karibuni kikundi kinachoongozwa na mtafiti Wu kilitengeneza vyembe vya kaboni vyenye kipenyo cha nanomita kadhaa kwa kutumia takataka za kadibodi, ambavyo vinaweza kubeba na kusambaza vyembe vya chuma cha zero-valent vyenye kipenyo cha nanomita kadhaa. Habari zinasema rasilimali hiyo ya mseto inaweza kuondoa Hexavalent chromium majini, na kuizuia metali hiyo kuhama au kuvutwa na mimea. Jambo lingine muhimu ni kwamba rasilimali hiyo ni rahisi kuzalishwa kwa gharama nafuu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako