• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Idadi ya wahamiaji haramu waliofariki baada ya boti waliyopanda kuzama nchini Tunisia yafikia 112

    (GMT+08:00) 2018-06-05 18:14:26

    Shirika la Uhamiaji la Kimataifa (IOM) limesema, idadi ya wahamiaji haramu waliofariki baada ya boti yao kuzama kwenye pwani ya kusini mashariki mwa Tunisia jumapili imefikia 112.

    Awali, vyombo vya habari nchini humo viliripoti kuwa boti hiyo ilikuwa na wahamiaji haramu 180 wakiwemo 80 kutoka nchi nyingine za Afrika.

    Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Ndani wa Tunisia Bw. Khalifa Chibani amesema vikosi vya usalama vya nchi hiyo vinawashikilia watu wanane wanaoshukiwa kuratibu safari hiyo katika kisiwa cha Kerkennah jumamosi jioni.

    Katika mwaka mmoja uliopita, Tunisia imekuwa njia mpya muhimu kwa wahamiaji wanaojaribu kwenda Ulaya, na Kerkennah inajulikana kama moja ya njia kuu isiyo halali inayotumiwa na wahamiaji haramu.

    IOM imesema, tangu mwanzo wa mwaka huu, karibu wahamiaji 1,910 wa Tunisia wamefikia Italia kwa kutumia njia ya bahari.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako