• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yatoa kanuni ya maadili ya mazingira ya kiekolojia ya raia

    (GMT+08:00) 2018-06-05 19:15:52

    Leo ni siku ya kimataifa ya mazingira.

    China imeweka kaulimbiu ya siku hiyo kuwa "China yenye madhari safi, mimi ni mtendaji" ambapo Wizara ya mazingira ya China na idara nyingine zimetangaza kwa pamoja Kanuni ya Maadili ya Mazingira ya Kiikolojia ya Raia.

    Kanuni hizo ni pamoja na kufuatilia mazingira ya kiasili, kubana matumizi ya nishati, kufanya matumizi yanayofaa mazingira, kuchagua usafiri usioharibu mazingira, kugawa takataka kwa aina tofauti, na kupunguza uzalishaji wa uchafuzi, kulinda mazingira ya kiasili, kushiriki kwenye usimamizi na kujenga China yenye mandhari safi.

    Waziri wa mazingira Bw. Li Ganjie amesema, kila mtu anapaswa kuwa mfuatiliaji wa ulinzi wa mazingira, kufuatilia sera ya mazingira ya asili na kutoa pendekezo kwa serikali. Pia kila mmoja kuwa msimamizi wa masuala ya mazingira, kugundua masuala ya uharibifu wa ikolojia na uchafuzi wa mazingira, na kuyazuia au kuripoti masuala hayo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako