• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais Putin atarajia mkutano wa viongozi wa Marekani na Korea Kaskazini utapata mafanikio

    (GMT+08:00) 2018-06-06 07:31:37
    Rais Vladmir Putin wa Russia amesema anatarajia mafanikio yatapatikana katika mkutano ujao wa viongozi wa Marekani na Korea Kaskazini, na Russia pia itafanya juhudi zote kufanikisha mkutano huo.

    Rais Putin amesema msimamo wa China na Russia kwenye suala la nyuklia la peninsula ya Korea Kaskazini unafanana, na pande hizo mbili zimetoa mpango wa kutatua suala hilo. Russia inaunga mkono kikamilifu jitihada za China katika kutuliza hali ya kanda hiyo.

    Rais Putin amepongeza uamuzi wa Korea Kaskazini kusimamisha majaribio ya makombora na silaha za nyuklia, ambao ni hatua kubwa katika kutimiza lengo la kuondoa silaha za nyuklia katika peninsula ya Korea.

    Akizungumzia uhusiano wa Russia na nchi za magharibi, rais Putin amesema Russia siku zote inafuata njia ya kujiendeleza kwa kujitegemea na kujiamulia, na haiogopi vikwazo vyovyote, na njama yoyote ya kukwamisha maendeleo ya Russia kupitia kuiwekea vikwazo haitafanikiwa. Amesisitiza kuwa Russia inatarajia kudumisha uhusiano mzuri na nchi za magharibi ikiwemo Marekani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako