• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Chama tawala cha Afrika Kusini chaonya wanaotumia mitandao ya kijamii kushambulia wengine

    (GMT+08:00) 2018-06-06 09:24:59

    Chama cha tawala cha Afrika Kusini ANC kimetoa onyo kali kwa wanachama wanaotumia mitandao ya kijamii kufanya mashambulizi binafsi na kutoa matusi dhidi ya wengine. Onyo hilo limetolewa baada ya meya wa manispaa ya Dihlabeng kumtukana Rais Cyril Ramaphosa kupitia ukurasa wa Facebook.

    Taarifa iliyotolewa na ANC inasema chama hicho kinalaani vikali matusi dhidi ya Rais Ramaphosa toka kwa viongozi wa ANC na hata wanamtandao. Msemaji wa ANC wa taifa Bw. Pule Mabe amesema watu wanaweza kutoa maoni yao binafsi bila kushambulia watu binafsi au kutoa matusi. Pia amesema hivi karibuni ANC ilitoa sera inayowazuia wanachama wake kutumia lugha ya matusi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako