• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Vifo kutokana na uzazi vyazidi vya Malaria na TB Afrika Magharibi

    (GMT+08:00) 2018-06-06 09:25:19

    Ripoti iliyotolewa jana na Shirika la Afya la nchi za Afrika Magharibi WAHO, imesema idadi ya vifo wakati wa uzazi katika eneo la Afrika magharibi ni kubwa kuliko idadi ya vifo vinavyotokana na magonjwa ya kitropiki kama vile Malaria na kifua kikuu.

    Ofisa afya mwandamizi wa WAHO Bw. Salofou Zouma, amewambia wajumbe kutoka nchi 14 wanachama wa ECOWAS, kuwa mwaka jana vifo zaidi ya elfu 5 viliripotiwa kutoka katika vituo vya afya. Amesema licha ya kuwa idadi hiyo ni makadirio ya chini kutokana na kutokamilika kwa ripoti, idadi hiyo imezidi magonjwa yote ya kitropiki kwenye eneo hilo.

    Hata hivyo amesema magonjwa ya malaria na kifua kikuu bado yanaendelea kuwa hatari katika eneo hilo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako