• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Watu 15 wamefariki dunia kutokana na ugonjwa wa kipindupindu magharibi mwa Tanzania

    (GMT+08:00) 2018-06-06 09:25:38

    Watu 15 wamefariki dunia na wengine 397 wamelazwa katika muda wa wiki tatu zilizopita kutokana na mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu wilayani Sumbawanga, magharibi mwa Tanzania.

    Ofisa afya wa wilaya ya Sumbawanga Bw Fani Mussa amesema wataalamu wa afya wanaendelea na juhudi za kuimarisha juhudi za kukabiliana na ugonjwa huo.

    Amesema chanzo cha kuenea kwa mlipuko wa ugonjwa huo kinatokana na jamii ya huko kupuuza hatua za usafi. Amesema mlipuko wa safari hii umetokana na wakazi kunywa maji yasiyo salama wakati wa mavuno ya mpunga.

    Hii sio mara ya kwanza kwa kipindupindu kutokea katika eneo hilo. Mwezi Novemba mwaka jana watu 7 walifariki kutokana na ugonjwa huo, kabla ya kudhibitiwa mwezi machi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako