• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ndege iliyokuwa na abiria 10 yapotea Kenya

    (GMT+08:00) 2018-06-06 09:44:43

    Ndege ndogo iliyokuwa na abiria 10 ikisafiri kutoka mji wa Kitale magharibi mwa Kenya kuelekea Nairobi imepotea.

    Mkurugenzi mkuu wa mamlaka ya usafiri wa anga ya Kenya KCAA Bw. Gilbert Kibe, amesema ndege hiyo aina ya ya Cessna C208 ilionekana kwenye Rada kwa mara ya mwisho saa 8 mchana.

    Habari zinasema ndege hiyo inadhaniwa kuanguka karibu saa 11 jioni, kilomita 40 baada ya kuruka kutoka Kitale.

    Kikosi cha uokoaji kimetumwa lakini kazi yao inakwamishwa kutokana na hali mbaya ya uonaji kwenye eneo la tukio.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako