• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Watu watano wauawa katika shambulizi la kundi la al-Shabaab Somalia

    (GMT+08:00) 2018-06-06 09:52:20

    Watu wasiopungua watano wameuawa na wengine kadhaa wamejeruhiwa katika shambulizi lililofanywa na kundi la al-Shabaab dhidi ya msafara wa kijeshi karibu mji wa Balad, kilomita 30 kaskazini mwa Mogadishu.

    Ofisa wa polisi wa Somalia amesema shambulizi hilo liliulenga msafara uliokuwa na wabunge wa eneo hilo na maofisa wa serikali. Kati ya watu watano waliouawa kuna wabunge na askari, na idadi hiyo huenda ikaongezeka.

    Wakazi wa eneo la tukio wamesema walisikia mlipuko na sauti za risasi, na kutambua kuwa lilikuwa ni shambulizi lililofanywa na wapiganaji wa Al Shabaab.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako