• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Sudan yapendekeza kufanyika mazungumzo kati ya rais wa Sudan Kusini na kiongozi wa waasi

    (GMT+08:00) 2018-06-06 10:03:10

    Serikali ya Sudan imetoa pendekezo la kufanyika kwa mazungumzo kati ya rais Salva Kiir wa Sudan Kusini na kiongozi wa kundi la waasi Bw. Riek Machar.

    Wizara ya mambo ya nje ya Sudan imetoa taarifa ikisema ujumbe wa ngazi ya juu wa Sudan umefanya ziara mjini Juba Sudan Kusini, na kufikisha ujumbe wa rais Omar al-Bashir wa Sudan kwa rais Salva Kiir wa Sudan Kusini.

    Taarifa imesema ujumbe huo kutoka kwa rais Omar al-Bashir unahusu pendekezo la kuunga mkono kutimiza amani kati ya rais wa Sudan Kusini na kiongozi wa kundi la waasi, na unaonyesha dhamira ya Sudan ya kuendesha mazungumzo kati ya pande hizo mbili za Sudan Kusini.

    Rais Salva Kiir wa Sudan Kusini amefurahia pendekezo hilo, na kusisitiza tena kuwa serikali yake inapenda kushiriki na kuyafanikisha mazungumzo hayo, ili kutimiza usalama na utulivu nchini Sudan Kusini.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako