• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Balozi mpya wa China nchini Kenya aahidi kuimarisha uhusiano kati ya China na Kenya

  (GMT+08:00) 2018-06-06 10:18:11

  Balozi mpya wa China nchini Kenya Bibi Sun Baohong ameahidi kutumia nafasi yake kuimarisha uhusiano kati ya China na Kenya, ili kukuza zaidi ushirikiano wa kimkakakti uliopo kati ya nchi mbili.

  Bibi Sun ambaye ni balozi wa kwanza mwanamke wa China nchini Kenya, aliyasema hayo alipokabidhi hati zake kwa rais Uhuru Kenyatta wa Kenya mjini Nairobi.

  Taarifa iliyotolewa na ikulu ya Kenya inasema China na Kenya zimekuwa na ushirikiano wa miaka mingi katika sekta mbalimbali ikiwemo ujenzi wa miundo mbinu na viwanda. Kenya imesema inakaribisha uwekezaji wa China katika sekta ya viwanda kwa kutumia teknolojia, fedha, na uzoefu wa China ili kuhimiza ukuaji wa viwanda kama ilivyopangwa kwenye ruwaza yake ya mwaka 2030.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako