• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Waziri mkuu wa Misri akabidhi barua ya kujiuzulu kwa baraza lake la mawaziri

    (GMT+08:00) 2018-06-06 18:36:20

    Kituo cha televisheni cha taifa la Misri jana kimesema, waziri mkuu wa nchi hiyo Bw. Sherif Ismail amemkabidhi rais Abdel Fattah al-Sisi barua ya kujiuzulu kwa baraza lake la mawaziri.

    Rais al-Sisi ameagiza serikali ya sasa kuwa serikali ya mpito, ambayo itaendelea kutekeleza majukumu hadi serikali mpya itakapoundwa.

    Tarehe 2 mwezi huu, rais al-Sisi aliapishwa kuwa rais wa Misri, na atakuwa madarakani kwa kipindi cha pili cha miaka minne wa urais.

    Kwa mujibu wa taratibu, rais atateua waziri mkuu mpya ambaye ataidhinishwa na bunge, na waziri mkuu huyo ataunda baraza lake la mawaziri, ambapo baadhi ya mawaziri wataidhinishwa baada ya kushauriana na rais.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako